Katibu mkuu huyo alikuwa akijibu swali lililomtaka kueleza njia atakazotumia kusaka suluhu ya mchakato wa Katiba baina ya chama chake na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kama alivyoagizwa na Kamati Kuu (CC) ya CCM iliyofanyika juzi.
Kamati Kuu ilitoa agizo hilo baada ya kupokea
taarifa tatu za mwenendo wa mchakato wa Katiba zilizowalishwa na Kinana,
Katibu wa Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wa CCM ambaye pia ni Waziri wa
Katiba na Sheria, Dk Asha-Rose Migiro na Katibu wa Wabunge wa CCM na
Naibu Waziri Elimu naMafunzo ya Ufundi, Janister Mhagama
.
.
“Kuna njia mbili kubwa za kuendelea kusaka
maridhiano; kwanza ni kupitia Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) na
Baraza la Vyama vya Siasa ambako kuna fursa za viongozi wa vyama
kujadiliana masuala mbalimbali licha ya tofauti za mitizamo na itikadi
za vyama vyetu,” alisema Kinana na kuongeza:
“Tumekuwa tukizungumza na kuna kila dalili ya
kupata mwafaka licha ya kwamba siyo lazima mwafaka huo uwalazimishe
waliotoka kurejea bungeni, lakini jambo la msingi lazima tuhakikishe
mazingira ya kuendesha siasa zetu ni salama kwa faida ya vyama vyetu
nchi yetu.
”
”
Alisema mbali na suala la kuwashawishi Ukawa
warejee bungeni, majadiliano ya vyama vya siasa pia yanalenga kujadili
jinsi ya kujenga mazingira sawa ya uendeshaji wa siasa, hasa katika
kipindi hiki Taifa linapoelekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2015.
Kinana alisema pamoja na kuvunjika kwa mazungumzo
yaliyokuwa yakiratibiwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis
Mutungi anaamini TCD ni sehemu mwafaka kwani inajumuisha viongozi wa
vyama ambavyo siyo sehemu ya mvutano uliopo.
Taarifa za ndani
Kauli ya Kinana inashabihiana na habari kutoka
ndani ya chama chake ambazo zimekuwa zikidai kwamba chama hicho tayari
kimefanya mazungumzo na wapinzani kwa ajili ya kuifanyia marekebisho ya
Katiba ya sasa ili kujenga mazingira ya usawa katika Uchaguzi Mkuu ujao
.
.
Tayari vyama vya upinzani vimependekeza mambo
manne yanayopaswa kuzingatiwa katika mabadiliko hayo ambayo ni kuwapo
kwa Tume Huru ya Uchaguzi, Matokeo ya urais kuhojiwa Mahakamani,
kuruhusiwa kwa mgombea binafsi na mshindi wa urais kupata kura zaidi ya
asilimia 50 tofauti na sasa.
Katika muktadha huo, ndiyo maana Ukawa wamekuwa na
msimamo wa kutaka Bunge hilo lisitishwe kusubiri mwafaka, jambo ambalo
hata hivyo, Kinana alisema ni ngumu kutekelezwa kwa sababu sheria
imefunga milango kuhusu suala hilo
No comments:
Post a Comment